26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Sarri njiani kuondoka Chelsea

LONDON, England

MAMBO mengi lakini muda ni mchache, baada ya kocha wa kikosi cha Chelsea, Maurizio Sarri kuwaambia mabosi wake kuwa anataka kuondoka ndani ya timu hiyo.

Sarri hivi karibuni amesaidia timu ya Chelsea kutwaa taji la Europa, baada ya kuichapa mabao 4-1 Arsenal, kwenye Uwanja wa Olmpiki uliopo katika Mji wa Baku.

Hivi karibuni, kituo cha michezo nchini England, Sky Sports kiliripoti kuwa kocha huyo raia wa Italia anawindwa vikali na Juventus ambao wamemtimua Massimiliano Allegri, baada ya msimu kumalizika.

Sarri alikutana na mkali wake anayefahamika kwa jina la Fali Ramadani na kumweleza kuwa hana mpango wa kuendelea kuwepo ndani ya timu ya Chelsea.

Ndani ya msimu wake mmoja ambao alikuwa ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake Stamford Bridge, amefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na kutwaa taji la Europa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles