27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

USIYOYAJUA KUHUSU PASCAL WAWA

NA MWAMVITA MTANDA

WAKATI anakanyaga ardhi ya Tanzania  kwa mara nyingine ili kusaini mkataba Simba, asilimia kubwa ya mashabiki wa soka hawakuwa na imani naye  tena na uwezo wake dimbani.

Wengi waliamini kwamba, muda wake wa kutundika daruga umefika na pengine tamaa ya fedha tu ndiyo inayomlazimisha kuendelea kucheza soka.

Ninayemzungumzia hapa si mwingine, bali ni  beki wa kati raia wa Ivory Coast, Pascal Serge Wawa.

Inawezekana mashabiki wengi wa soka wanafahamu maisha yake ya soka, lakini nje ya soka hawajui chochote kuhusu beki huyu kisiki.

Kwa  kuliona hilo MTANZANIA limefanya jitihada za  kumtafuta Wawa na kuzungumza naye,  ili kutaka kufahamu maisha yake ya nje ya dimba, na baada ya kufanikiwa kumpata hivi ndivyo ilivyokuwa;

 MTANZANIA  : Pascal Wawa habari yako? 

WAWA: Niko poa sana niambie. 

MTANZANIA :Kwanini unafuga ndevu nyingi hivyo? 

WAWA: hahaha! Kwetu Ivorycost ukifuga ndevu kama zangu hivi unaonekana ni mfalme na mtu mwenye heshima kubwa sana. 

Mtanzania: Na hizo tatuu vipi hazina madhara,  mbona umechora nyingi sana?

WAWA: Unajua katika maisha kila mtu hupenda kufanya anachokipenda, tatuu haina madhara lakini hapa kila mchoro unamaana yake . Na kikubwa zaidi ni heshima katika kazi yangu . Pia hizi tatuu zinanifanya nijione mwenye nguvu kama mwanaume mpambanaji.

 MTANZANIA : Una watoto wangapi?

WAWA:Kwanini unaniuliza maisha yangu ya ndani?

 MTANZANIA:Hakuna tatizo na hitaji kufahamu tu . 

WAWA: Namshuru Mungu nimebahatika kupata watoto watano,wa kike na wakiume. 

MTANZANIA : Hongera sana, watoto wako wote wanatokana na  mama mmoja au umechanganya damu?

WAWA: Hapana, mama yao ni mmoja, kwa kuwa huwa naamini watoto wakizaliwa pamoja wanapata malezi mazuri ya baba na mama.

 MTANZANIA :Unapendelea kuwa na marafiki wa aina gani?

 WAWA: Kwanza mimi sina marafiki ila ninao washkaji wengi ambao tunaelewana hapa Tanzania na nchini kwetu, lakini rafiki yangu wa karibu ni bibi mmoja ambaye naishi nae hapa anaitwa Fabregas.

MTANZANIA : Siku za mapumziko huwa unapenda kufanya nini?

WAWA: Napenda kuenjoy(kujifurahisha) kwa  kuogelea ufukweni,ili nipumzishe akili na kuweka sawa mipango yangu ya kimaisha.

 MTANZANIA: Kutokana na umaarufu wako katika soka, nje na ndani ya Tanzania,  je unapata usumbufu kutoka kwa warembo?

 WAWA : Sanaa! napata usumbufu mkubwa ,lakini najitahidi kujizuia ukizingatia mimi ni baba wa familia ambaye nategemewa hivyo lazima nijilinde.

 Natambua kile ambacho nimekuja kukifanya Tanzania, nipo kazini nikianza kuwa karibu na kila mwanamke nitakuwa na matumizi mabaya ya pesa na sitafikia malengo.

 MTANZANIA: Lakini unampenzi hapa Tanzania ?

WAWA: Hahaha wewe una maswali mengi, mimi mina mke wangu tu,  mama wa watoto wangu na huwa anakuja kunitembelea na mimi pia likizo huwa naenda .

MTANZANIA:Unapendelea kula chakula cha aina gani?

 MTANZANIA : Napenda kula makange na wali samaki,  napenda sana.

MTANZANIA: Aina gani ya kinywaji unapendelea kutumia?

WAWA: Napenda kunywa juisi ya pasheni. 

MTANZANIA: Vipi kuhusu matumizi ya kilevi? 

WAWA : Hapana, kutokana na kazi yangu kilevi ni hatari kwa afya, ila naweza kunywa vinywaji laini. 

MTANZANIA: Mwanamke wa aina gani ukimuona lazima ugeuke?

 WAWA: Daaah! mnene au mweupe.

 MTANZANIA : Watoto wako unapenda wawe akina nani  hapo baadae?

WAWA: Kwa upande wa watoto wa kiume , napenda waje kufanya kazi kama yangu, lakini wakike wafanye kazi zingine ,lakini wote nataka wasome kwa bidii sana.

 MTANZANIA : Unazunmza lugha ngapi?

 WAWA: Nazungumza kifaransa, ni kama lugha mama ya kwetu, Kingereza na kiswahili kidogo sana.

 MTANZANIA : Nakushukuru sana Pascal Wawa kwa muda wako Mungu akubariki .

 WAWA: Asante na karibu tena

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles