LOS ANGELES, MAREKANI
MWIGIZAJI wa filamu wa Marekani, Sarah Hyland, ameweka wazi sababu za kifo cha mpwa wake, Trevor Canaday, kuwa aliuawa na dereva ambaye alikuwa akiendesha gari huku akinywa pombe.
Canaday, alifariki dunia juzi kwa ajali ambayo inadaiwa kusababishwa na ulevi.
Akielezea katika ukurasa wake wa Instagram, Hyland alisema: “Huyu ni mpwa wangu ana umri wa miaka 14, jana (juzi) aliuawa na dereva aliyekuwa akinywa pombe huku akiendesha gari. Mjomba wangu bado yupo hospitali akiendelea kufanyiwa upasuaji kutokana na ajali hiyo.
“Trevor alikuwa mcheshi, mnyenyekevu na kijana mweye tabia nzuri.”