Mourinho amfukuzisha kazi kocha Southampton

0
2004

LONDON, ENGLANDUONGOZI wa Southampton umemfuta kazi kocha wake, Mark Hughes, baada ya kufanya vibaya katika michezo 14 ya Ligi Kuu England msimu huu.

Katika michezo hiyo, Southampton imeshinda mchezo mmoja dhidi ya Swansea kabla ya kupoteza nafasi ya kushinda mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United ambao ulimalizika kwa kufungana mabao 2-2 Jumapili iliyopita.

Vijana wa Hughes walikuwa wakiongoza mchezo kwa mabao 2-0 baada ya dakika 20 lakini Manchester United ilisawazisha mabao yote kabla ya kipindi cha pili kumalizika.

Baada ya mchezo huo uliochezwa juzi, klabu ya Southampton, ilimtimua Hughes na wasaidizi wake wawili, Mark Bowen na Eddie Niedzwiecki.

Nafasi ya Hughes, itachukuliwa na aliyekuwa kipa wa zamani wa timu hiyo, Kelvin Davis, ambaye ataanza kazi ya kuifundisha timu hiyo katika mchezo dhidi ya Tottenham, utakaochezwa kesho katika Uwanja wa St Mary, London, England.

Kwa sasa klabu hiyo ipo katika mazungumzo na aliyekuwa kocha wa RB Leipzig, Ralph Hasenhüttl, ambaye anapewa nafasi ya kuchukua mikoba ya kuifundisha timu hiyo moja kwa moja.

Hasenhüttl, amepewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba hiyo baada ya kuwavutia mabosi wa Southampton.

Southampton, ambayo imethibitisha kuondoka kwa Hughes jana, inafahamu kuwa ilikuwa katika mazungumzo ya awali na kocha wa RCD Espanyol, Quique Sanchez Flores na kocha wa Tianjin Quanjian FC, Paulo Sousa, hivyo watalazimika kutoa msimamo wao kabla ya mchezo dhidi ya Cardiff City.

Hasenhuttl pia aliwahi kuhusishwa kutakiwa na klabu ya Arsenal na Brentford baada ya kuachia ngazi kuifundisha Leipzig Mei mwaka huu.

Aina yake ya ufundishaji inadaiwa kufanana na kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here