26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Sanamu ya Ronaldo yawekwa jina la Messi

Ronaldo sanamuMADEIRA, URENO

SANAMU ya nyota wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ambayo ipo katika mji wa Madeira nchini Ureno, imekutwa na jina la Lionel Messi.

Jina hilo na namba ya jezi ya Messi (10), limeandikwa na watu wasiojulikana mara baada ya Messi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya Ballon d’Or, Jumatatu wiki hii.

Inasemekana kwamba, kuna baadhi ya mashabiki wa Messi katika mji huo, hivyo baada ya mchezaji huyo kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kulikuwa na furaha kubwa kwa baadhi ya mashabiki ambao walikuwa wanapita katika sanamu hiyo ya Ronaldo.

Sanamu hiyo iliwekwa mwaka 2014 kwa heshima ya mchezaji huyo wa Ureno kutokana na kulitangaza taifa hilo duniani.

Hata hivyo, dada wa Ronaldo, Katia Aveiro, alimechukizwa na kitendo hicho cha kuichafua sanamu ya kaka yake kwa kuandika jina la Messi na namba ya jezi yake.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katia aliwatupia lawama mashabiki wa Messi katika mji huo na kudai kwamba wao wamehusika kuichafua sanamu hiyo ya heshima.

“Ni kitendo cha aibu sana watu kuchafua sanamu ya heshima, watu wataendelea kumpa heshima yake kutokana na kile ambacho anakifanya na wataendelea kumpigia kura.

“Analitangaza vizuri taifa hili lakini kuna watu wanajifanya hawajui umuhimu wake, ataendelea kuwa nyota wa Taifa hili,” alisema Katia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles