29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Rihanna, Drake wanaswa tena

drake na rihannaLOS ANGELES, MAREKANI

MPENZI wa zamani wa msanii wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, Rihanna Fenty ‘Rihanna’, amekutwa tena akiwa na mkali wa hip hop wa kundi la Young Money, Aubrey Graham ‘Drake’ wakiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Awali baada ya Chris kuachana na mrembo huyo, Drake alidaiwa kudondokea kimapenzi kwa mrembo huyo kiasi cha kukosana na Chris Brown lakini baada ya kimya kirefu juzi walionekana tena wakiwa pamoja katika maduka ya Eagle Rock Plaza Mall ambapo walipiga picha pamoja na mambo mengine yaliyowashangaza mashabiki wao waliokuwa eneo hilo.

Baada ya kuonekana huko Drake ali ‘post’ picha katika akaunti yake ya Instagram akaandika kwamba yeye na Rihanna wapo katika mpango wa kuandaa video yao mpya, hakuna la zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles