22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Samih Nuhu, Fakhi watua Simba

POPENA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

USAJILI wa klabu ya Simba sasa umeziingilia timu za Azam FC na JKT Ruvu, baada ya juzi kunasa mabeki wawili wakitokea klabu hizo ili kuongeza uimara wa ukuta wa timu yao.

Mabeki hao ni Samih Hajji Nuhu aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Azam msimu wa 2013/2014 anayecheza beki ya kushoto ambaye wamempa mkataba wa mwaka mmoja na Mohammed Fakhi wa JKT Ruvu akiwa ni beki kati aliyeanguka saini ya miaka miwili.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya timu hiyo, Zacharia Hanspoppe alisema, uwezo wa wachezaji hao ndio umewafanya wawaongeze katika kikosi chao hicho.

Alisema, usajili walioufanya hadi sasa ni kwa mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo kulingana na jinsi wao walivyoona uwezo wao kwani katika kipindi chote cha ligi licha ya kuhakikisha wanapata ushindi, pia walikuwa wakiangalia nani anawafaa kwenye usajili wa msimu ujao.

“Kwa upande wa Nuhu ambaye alikuwa ni majeruhi tumejiridhisha na vipimo vyake na vimeonyesha ni mzima kabisa, hivyo tunategemea mambo mazuri kutoka kwao,” alisema.

Usajili wa wawili hao umefanya idadi ya wachezaji wapya wa timu hiyo kufikia watatu, baada ya wiki iliyopita kumsajili kiungo wa Mbeya City, Peter Mwalyanzi.

Makakati wa klabu hiyo ni kuacha wachezaji 10, saba wa ndani na watatu wa kigeni ambao tayari wameshajulikana huku bado kuna sintofahamu kuwa kati ya hao wa kigeni nani anaachwa na yupi anatolewa kwa mkopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles