25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

SAMIA: MAOFISA UGANI SIMAMIENI UZALISHAJI WA NDIZI

Na ELIUD NGONDO, MBEYA               |             


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Mbeya kuwasimamia maofisa ugani ili waweze kuzalisha zao la ndizi kitaalamu kwa ajili ya ushindani kwenye soko la nchi za kusini mwa Afrika.

Samia alitoa kauli hiyo wilayani Kyela jana katika mwendelezo wa ziara yake ya Mkoa wa Mbeya.

Alieleza kusikitika baada ya kipatiwa taarifa kuwa raia kutoka nchi jirani wamekuwa wakinunua ndizi wilaya za Rungwe, Ileje na Kyela kisha zinafungwa kwenye vifungashio vizuri na kuzipeleka nchi za nje.

Alisema Wilaya ya Kyela ilistahili kuwa na  soko la kimataifa la zao la ndizi kwa ajili ya nchi za Kusini mwa Afrika.

“Naiagiza Serikali ya Mkoa wa Mbeya kuwashusha maofisa ugani waje wilayani  Kyela kwa ajili ya uzalishaji wa zao la ndizi, ili kuweza kuzalisha idadi ya kutosha na kisha kuzifunga na kuziuza nchi jirani zinazozunguka mikoa hii ya Songwe na Mbeya,” alisema Samia.

Aliongeza  kuwa ujenzi wa meli za kubeba mizigo ni fursa kubwa ya kuchochea shughuli za kiuchumi kwa kukusanya mapato pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania.

Awali akipokea taarifa ya ujenzi wa meli tatu zinazojengwa na Kampuni ya Songolo Milen, Samia alisema meli hizo ni fursa kubwa ya kibiashara kwa wananchi hivyo wanatakiwa kujituma katika uzalishaji wa mazao ya biashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles