24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

MAJALIWA ATAKA WADAU WA KILIMO KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI

Na Editha Karlo, Kigoma       |         


WAZIRI Mkuu, Kassimu Majaliwa, amewataka wadau wa zao la mchikichi nchini kuhakikisha wanafufua na kuendeleza zao hilo.

Majaliwa alitoa ushauri huo jana wakati akizungumza na wadau wa zao hilo katika ukumbi wa mikutano wa NSSF  uliopo mjini Kigoma, ambapo alisema zao la michikichi nchini lipo na si kwamba liaanza kulimwa, hivyo kupitia mkutano huo amewataka wananchi wa Kigoma kulifanya zao hilo  kama zao lao la kudumu.

Katika muktadha huo aliwataka wakurugenzi pamoja na maofisa kilimo katika halmashauri za mkoa huo kusimamia ipasavyo kilimo cha zao hilo tofauti na hivyo watawajibishwa.

“Zao la mchikichi ni muhimu kwa kuwa ni nikichocheo kikubwa cha  uchumi wa viwanda,  katika Mkoa wa Kigoma tukilima kwa wingi wenye viwanda watahamasika kuja na kuweka viwanda hapa kwa sababu watakuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi,” alisema Majaliwa.

Aliwataka maofisa ugani wote kuhakikisha wanawaelekeza wakulima kulima kitaalamu zao hilo  ili waweze kupata mazao yaliyo bora.

Alisema kwa sasa msisitizo wa Serikali ni kila mwananchi wa Mkoa wa Kigoma kupanda miche ya mchikichi  kwa sababu mpango uliopo ni kulifanya zao hilo kuwa la biashara kama ilivyo kwa mazao ya pamba, kahawa, korosho na tumbaku.

Katika kikao hicho wadau pia waliazimia kuwa na kituo cha utafiti cha zao la michikichi katika Mkoa wa Kigoma, ambapo wajumbe katika kikao hicho walipendekeza kituo hicho kiwe katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Kihinga ambacho kina ekari 300.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,859FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles