28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Samia kuzindua jukwaa la uchumi  leo Dar

Suluhu HassanNa Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere,  Dar es Salaam.

Uzinduzi wa jukwaa hilo utafanyika pamoja na uzinduzi wa Akaunti ya Malaika kwa ajili ya kuwafungulia akaunti wanawake wajasiriamali wadogo   nchini.

Hafla hiyo inategemewa kuhudhuriwa na watu wapatao 1,000 kutoka makundi ya wadau mbalimbali wakiwamo wanawake wajasiriamali wa Tanzania Bara na Visiwani.

Jukwaa hilo litatoa uelewa kwa washiriki hususan kuhusu fursa zilizopo na mikakati ya kumuwezesha mwanamke katika uchumi  na juhudi zinazofanywa na serikali katika  harakati za kuinua wanawake katika uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles