MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Uzinduzi wa jukwaa hilo utafanyika pamoja na uzinduzi wa Akaunti ya Malaika kwa ajili ya kuwafungulia akaunti wanawake wajasiriamali wadogo nchini.
Hafla hiyo inategemewa kuhudhuriwa na watu wapatao 1,000 kutoka makundi ya wadau mbalimbali wakiwamo wanawake wajasiriamali wa Tanzania Bara na Visiwani.
Jukwaa hilo litatoa uelewa kwa washiriki hususan kuhusu fursa zilizopo na mikakati ya kumuwezesha mwanamke katika uchumi na juhudi zinazofanywa na serikali katika harakati za kuinua wanawake katika uchumi.