28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Samia anafaa kuwa mgombea mwenza – Pinda

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Waziri Mkuu Mizengo Pinda

NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amempigia ‘debe’ Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samia Suluhu Hassan, kuwa ni mwanamke shupavu anayeweza kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka  2015.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana wakati wa kutoa shukrani, Pinda alisema Samia amepewa sifa kubwa kutokana na kazi nzuri aliyofanya ya kuliongoza Bunge hilo kwa uadilifu.

“Makamu mwenyekiti leo umepewa sifa kubwa, nimeambiwa unafaa kuwa mgombea mwenza, umefananishwa na simba jike, mimi kwa sababu natokea Katavi, najua kwenye mbuga hiyo simba jike anakuwaje,” alisema Pinda.

Alisema hatua iliyofikiwa na Bunge Maalumu la Katiba ni ya kutafakari kwa kina kwani kazi hiyo imefanywa na watu wengi na anaamini kuwa sauti ya wengi ni ya Mungu.

Pinda alisema wingi wa watu wanaoikubali Rasimu ya Katiba inayopendekezwa ni kielelezo tosha cha umoja wa wananchi japokuwa jitihada nyingi zinaendelea nje ya Bunge kukwamisha zoezi hilo.

“Watanzania wenzangu Katiba hii ina mambo mengi, naomba mtakapoipata muisome, kwa upande wangu mimi sura ya pili imenivutia, inazungumzia mambo mengi ya kiuchumi na vitu vya msingi wanavyopaswa kujua Watanzania,” alisema Pinda.

Alisema Katiba hiyo kama itapatikana kwa wakati, mpango wa maendeleo wa miaka mitano pia utashabihiana nayo, hivyo ni vema kujipanga ili kuweza kufanya kazi kwa uadilifu katika kuitengeneza ili kukamilisha dhamira tuliyonayo.

KAULI YA SAMIA

Akizungumza na wajumbe wa Bunge hilo, Samia alisema hivi sasa ni mwanasiasa tofauti na alivyokuwa awali kutokana na kuliongoza Bunge bila kuyumba.

“Wakati ule nilikuwa mwanasiasa mwanaharakati, lakini sasa ni mwanasiasa kamili, maana tukiwa hapa mmenifunza mengi na ninawashukuru sana ndugu zangu,” alisema Samia.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles