24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

LHRC kuchunguza theluthi mbili ya Z’bar

Dk. Helen Kijo-Bisimba
Dk. Helen Kijo-Bisimba

NA GRACE SHITUNDU, DAR ES SALAAM
MKURUGE NZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba, amesema watafanya uchunguzi kubaini mazingira yaliyowezesha kupatikana kwa theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Zanzibar.

Alisema ingawa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa imepitishwa, theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar haijulikani inatokana na kura gani, kwani toka awali hesabu zilionyesha kura za wajumbe kutoka visiwani zisingefikisha idadi inayotakiwa.

“Pamoja na kupitishwa hiyo rasimu, bado kuna utata wamepataje theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar,  tutafuatilia tujue imetokea wapi, kwa hesabu tulizokuwa tunapiga kulikuwa hakuna uwezekano,” alisema Dk. Bisimba.

Aidha alisema hata hivyo bado wananchi wana nafasi ya kuchuja katika kura ya maoni kuangalia ni mambo yapi waliyatolea maoni waliyotoa yapo katika Rasimu ya Katiba hiyo inayopendekezwa na yapi yametolewa, na ndipo wafanye uamuzi.

“Wananchi waelewe kuwa kupitishwa kwa rasimu ya tatu si mwisho wa mchakato, bali tunawasubiri katika kura ya maoni,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

5 COMMENTS

  1. Katiba hii ni bomu kwelikweli, imepitishwa kibabe, hila, ujanja, pengine na rushwa huenda ilitumika lakini pia haina maridhiano. hakuna kitu kibay akama hila, na mwisho wa hila siku zote ni kuaibika. Kuna hatari ya kuaibika kwa wale walioipitisha katiba hii, usicheze na Mungu wa mbinguni!

  2. Kuhoji kwa nini theluthi mbili za Zanzibar zimepatikana kuna sababu yake ambayo haijasemwa hapa. Aidha kupatikana kwa kura hizo kwa kiasi kikubwa kulitokana na namna ambavyo takwimu ilichezwa/ilichezewa, bila kujali vigezo vingine vikiwemo uchama, umoja, uzalendo, woga, mizengwe, rushwa na kadhalika. Hakuna mwitiko wa wazi toka kwa watanzania wengi mara baada ya matokeo kutangazwa. Hii inaonesha kuwa watanzania wengi bado hawaelewi katiba ni nini. Na hata itakapoletwa kwa watanzania katiba hiyo itapita. Bado tunahitaji ukombozi.

  3. Watanzania tumepokea rasimu ambayo inaelezwa kuwa imekidhi matakwa ya kura lakini hoja ya wengi watanzania ni kuwa haiko katika maridhiano ya mambo ambayo yalipendekezwa na timu kuu ya mheshimiwa warioba iliyopewa majukumu hayo na waheshimiwa wakongwe wa siasa katika nchi hii na rais. Ni watu wa kuheshimika na wamekuwa katika siasa kwa muda mrefu sana. Mimi kwa kusikiliza kwangu tamko ni kuwa rasimu hiyo itapokelewa na mheshimiwa rais tarehe 8/10/2014. Mimi kama mimi na kwa maoni yangu kutoka katika nafsi yangu ni kumwomba mheshimiwa raisi wetu aliweza kuchukua nafasi yake akakaa na vyama vya upinzani na akawasikiliza na kisha akaeleza kuhusu kutoweza kusitisha ukomo wa kazi iliyokuwa inajadiliwa na bunge hadi tarehe 4/10/2014 iliyokuwa imewekwa kwa mujibu wa sheria. Tunashukukuru kila kitu kilienda ilivyotakiwa na rasimu ikapatikana. Ombi langu kwa mheshimiwa rais ni kuwa aipokee kama ni karatasi ya feasibility study fulani imefanywa na akipendezwa achukue hatua yeye mwenyewe kuitisha safu ya Mzee Warioba na safu ya Ukawa ili kuweka vema vile vifungu ambavyo vinafanya hii rasimu kuwa si ya maridhiano na kisha aitoe kwa wananchi kaw kupigiwa kura. Nina imani na uhakika endapo itafanyika hivi hakuna shaka tutaipata katiba nzuri na yenye maridhiano mema na kuzidi kuendeleza Tanzania yetu kwa hali ya upendo na amani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles