28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

SAMATTA AWASILI KUIVAA BOTSWANA

Na ELIZABETH JOACHIM – TUDARCO

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta, amewasili na kujiunga na kambi ya timu hiyo inayojiandaa kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Botswana, utakaochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa),  Taifa Stars inahitaji kupata ushindi ili kupanda katika viwango vya ubora vya shirikisho hilo.

Akizungumza jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema mbali na Samatta, mchezaji mwingine wa Stars, Simon Msuva, anayecheza soka nchini Morocco, alitarajiwa kuwasili usiku wa kuamkia leo kujiunga na wenzake.

Alisema kuelekea mchezo huo, maandalizi ya timu yako vyema, ambapo wachezaji wanafanya mazoezi asubuhi na jioni na kabla ya kuanza kwa kambi hiyo madaktari wa Stars waliwafanyia vipimo wachezaji, lakini hakuna aliyeonekana kuwa na tatizo kubwa la kumfanya akose mchezo huo.

Katika hatua nyingine, Alfred alisema timu ya Botswana inatarajia kuwasili Alhamis tayari kuwakabili Stars, ambapo timu hiyo itakuwa na msafara wa watu 27, ikijumuisha wachezaji 18 na viongozi  tisa.

“Botswana watafikia kwenye hoteli ya Urban Rose, Ijumaa jioni watafanya mazoezi katika Uwanja wa Uhuru, ambao ndio utatumika kwa ajili ya mchezo huo na maandalizi ya mchezo wote kwa ujumla yanakwenda vyema,” alisema Lucas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles