32.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

SALAMU ZA LEMA ZATUA MKUTANO WA MAJALIWA

pg-3-dec-4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa Arusha jana, wakati alipowasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuhutubia mkutano wa hadhara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

 

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA 

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Secilia Pareso (Chadema), amewasilisha salamu za Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, katika mkutano wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Pareso alimtaja Lema aliyefutiwa maombi yake ya dhamana juzi na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha katika ziara ya Majaliwa mkoani hapa tangu jana, ilikuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, kuomba viongozi waliokuwa meza kuu kusalimia wananchi kwa dakika tatu tu.

Mkutano huo wa Majaliwa ulifanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa jana.

Pareso aliyesimama baada ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Catherine Magige, kusailimia wananchi, alianza kwa kushukuru kwa Majaliwa kufika na kutembelea Arusha na alisisitiza kuwa maendeleo kwa wananchi yanapaswa kuletwa bila mtazamo wala itikadi za vyama.

“Wananchi nimewasiliana na Mbunge wenu Godbless Lema anaendelea vizuri ana afya njema na anawasilimia sana, tunaendelea kusubiria hadi hapo haki itapotendeka,” alisema Pareso na kulazimu kuibua shangwe kwa watu waliosimama mbele ya jukwaa kuu.

Kiongozi mwingine wa Chadema ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, alipewa nafasi kusalimia wananchi katika mkutano huo naye alitaka kuliteka jukwaa baada ya kuhamaisha wananchi kumsalimia Majaliwa.

Lazaro aliyefuatana na Majaliwa tangu juzi katika mkutano ya ndani na hata katika ziara viwandani akiwa kwenye mkutano huo aliwahamasisha wananchi kumsalimia Majaliwa kwa kupunguza mikono juu.

“Wananchi tumsalimie waziri mkuu kwa kupunguka mikono juu, nyanyua mkono juu twendeee Arusha safiiii, Waziri Mkuu oyeee,” alisema Lazaro huku akimuambia Majaliwa karibu Arusha na hili ndio Jiji linaloongozwa na meya bora Tanzania hatua iliyolazimu kuibua shangwe tena kutoka kwa watu.

Kwa upande wake, Gambo, akizungumza uwanjani hapo kabla ya kumkaribisha Majaliwa kuzungumza na wananchi alimpongeza Lazaro kwa kukubali kwenda na kasi ya Hapa Kazi Tu.

“Mheshimiwa waziri mkuu, sisi Arusha tunafanya kazi kama huko juu, hapa Arusha tulikuta madiwani wakiwa wanalipana posho kubwa ambazo hakuna madiwani wengine wanalipwa.

“Nashukuru meya tulimuelewa na akatuelewa hivyo tukalazimika kuziondoa posho za usafiri na vikao kisha fedha hizo tukazielekeza maeneo mengine ya maendeleo,” alisema Gambo.

Akizungumza kuhusu kero za maji na umeme, Majaliwa, alisema kero hizo sasa zinakwenda kutatuliwa baada ya Serikali kutenga kiasi cha Sh bilioni 476 kwa ajili ya mradi wa maji mkubwa mkoani humo.

Alisema Jiji la Arusha halipaswi kukatikatia umeme kutokana na kuwa na hadhi ya utalii.

“Tumeidhinisha shilingi bilioni 264 kwa ajili ya kuhakikisha umeme haukati Arusha, sasa Meneja wa Tanesco nikiskia umeme unaendelea kukatika baada ya mradi huu, itakuwa taabu,” alisema Majaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles