27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Salah atumia miezi mitatu kufunga bao moja

Mohamed SalahROMA, ITALIA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Roma ya nchini Italia, Mohamed Salah, ametumia miezi mitatu kufunga bao moja huku mara ya mwisho ikiwa ni Oktoba 25 mwaka jana.

Mchezaji huyo amekuwa na ukame wa mabao katika klabu hiyo, lakini juzi aliipatia klabu hiyo bao katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sassuolo katika michuano ya Ligi Kuu nchini Italia.

Hata hivyo, katika mchezo huo, Salah alionekana kuibeba timu yake kutokana na kasi ambayo aliitumia ambapo mashambulizi hayo yalizaa matunda baada ya mchezaji huyo kufunga bao la mbali.

Kwa upande mwingine, Roma ilifanikiwa kupata nafasi nyingi za kufunga mabao lakini walishindwa kuzitumia.
Hata hivyo, mlinda mlango wa klabu ya Sassuolo, Andrea Consigli, alionesha uwezo wake wa kuokoa mipira mingi ya hatari ambapo baadhi ya mipira hiyo ikipigwa na El Shaarawy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles