29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Klopp adai anahitaji muda kuiweka sawa Liverpool

jurgenkloppLIVERPOOL, ENGLAND

BAADA ya Liverpool kupokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Leicester City kwenye michuano ya Ligi Kuu nchini England juzi, kocha wa timu hiyo, Jurgen Klopp, amedai kwamba anahitaji muda kuijenga timu hiyo.

Katika mchezo huo, Liverpool walikuwa ugenini kwenye Uwanja wa King Power, ambapo waliambulia kichapo kutoka kwa vinara hao wa Ligi Kuu England wenye pointi 50 baada ya kucheza michezo 24.

Mabao ya Leicester City yaliwekwa wavuni na mshambuliaji wake hatari, Jamie Vardy katika dakika ya 60 na 71, huku bao hilo la pili likipigwa umbali wa mita 30 na kumchanganya kocha Klopp.

“Vardy amefanya siku iwe mbaya, amefunga mabao mazuri na yenye uwezo binafsi na anastahili kupewa sifa, kwa
upande wetu tulipata nafasi nyingi lakini wachezaji wangu walishindwa kuzitumia.

“Hii ni hali mbaya kwangu kutokana na matokeo haya nilijua nini kinatakiwa kufanyika, lakini wachezaji
hawakuweza kufanya hilo na ndiyo maana tumeupoteza mchezo huo.

“Bado tuna nafasi ya kuendelea kufanya vizuri kama tutakuwa na mshikamano na kikubwa ni kunipa muda ili
niweze kuitengeneza timu,” alisema Klopp.

Liverpool kwa sasa inashika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi huku ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza michezo 24, lakini kocha huyo anaamini kwa kipindi kilichobaki anaweza kuleta furaha katika klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles