25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Safari ya Pristorius kwenda jela illivyo kamilika

 Oscar Pistorius
Oscar Pistorius

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO,

Ilikuwa Februari 14, 2013, ikiwa ni siku ya wapendanao, mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius alimuua mpenzi wake mwanamitindo, Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi nne.

Pistorius mwenye umri wa miaka 29, amekuwa maarufu sana kutokana na kushinda baadhi ya medali ya katika michuano mbalimbali ya riadha, ikiwa mwaka 2012 ambapo alifanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Olimpiki kwa walemavu mjini London.

Kutokana na mauaji ya mpenzi wake, mwanariadha huyo alikamatwa bila ya kujali kuwa ni mlemavu wa miguu na watu wengi walishangaa nchini Afrika Kusini huku wakiamini kuwa yeye ni shujaa wa nchini kutokana na kuliwakilisha taifa katika mataifa mbalimbali.

Machi 3, 2014

Pristorius alifikishwa mahakamani kwa ajili ya shtaka lake, hata hivyo mwanariadha huyo alikana shtaka hilo baada ya kutoa utetezi wake chini ya Jaji Thokozile Masipa, akidai hakufanya mauaji hayo kwa makusudi bali alidhania ni majambazi wamewavamia.

Hata hivyo kutokana na utetezi wake mahakama hiyo ya mjini Pritoria, ilimuachia mwanariadha huyo kwa dhamana ya randi millioni moja, sawa na kiasi ya Dola 100,000. Hivyo kesi hiyo ilisogezwa mbele hadi mwaka uliofuata.

Aprili 10, 2014

Pistorius alirejea mahakamani kuhojiwa zaidi na kujibu maswali ya mwendesha mashtaka mkuu Gerrie Nel, juu ya kesi yake, hata hivyo mwendesha mashtaka huyo alionekana kumwandama Pistorius, huku akidai kwamba hakuwa mkweli katika maelezo yake.

Siku ya kwanza ya maswali ya mahakama dhidi yake Nel alianza kwa kuonyesha picha za kutisha za kichwa kilichochuruzika damu cha Bi Steenkamp, baada ya kupigwa risasi na Pistorius.

Kiongozi wa mashataka alimsuta sana Pistorious akisema kuwa alikuwa ni mbinafsi kwa mpenzi wake, ila Pistorious alikanusha madai hayo akisema anajuta kwanini hakuwahi kumwambia Reeva kuwa anampenda kupitia ujumbe wa simu ya mkononi. Ila viongozi wa mashtaka waliamini Pistorius aliua kwa kukusudia.

Mei 14, 2014

Jaji ambaye alikuwa anahusika na kesi ya Pristorius, alidai kwamba mwanariadha huyo anatakiwa apelekwe katika kituo cha afya kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kiakili, baada ya uchunguzi, mwanariadha huyo alidaiwa kuwa na maradhi yanayaohusiana na kuhangaika.

Jaji alisema kuwa ameridhika kwamba mtaalamu huyo ameshawishi mahakama kuruhusu mshitakiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi, ingawa hatua hiyo itachelewesha kuendelea kwa kesi hiyo.

Septemba 12, 2014

Kesi ya Pistorius iliendelea mahakamani hapo, lakini Jaji Thokozile Masipa, alidai kwamba mwanariadha huyo ameondolewa kosa la kuua bila kwa kukusudia na badala yake ikawa amemakosa ya mauaji, na badala yake Pistorious anakabiliwa na makosa ya kuua kwa kukusudia hivyo ikawa ameua bila kukusudia.

Hata hivyo mwendesha mashtaka aliendelea kusisitiza kuwa Pistorius alimpiga risasi Reeva wakati wa ugomvi baina yao lakini Pistorius amekuwa akijitetea kuwa alidhani ni mwizi aliyevamia nyumba yake, hivyo alikusudia.

Sheria ya kuua bila kukusudia nchini humo mtuhumiwa anaweza kwenda jela kwa miaka 15 au chini ya hapo na kuna muda anatakiwa kutumikia kifungo cha nje, hali hiyo iliwapa wasi wasi wengi ambao walikuwa wanafuatilia kesi hiyo kwa ukaribu.

Hata hivyo mwendesha mashtaka alidai kwamba mbali na mwanariadha huyo kudaiwa kuwa ameua bila kukusudia ila anatakiwa kukabiliwa na shtaka la matumizi mabaya ya bunduki.

Juni 13, 2016

Siku hii Pistorius alitakiwa kwenda mahakamani kwa ajili ya kesi yake, lakini alishindwa kutokana na kusumbuliwa na msongo wa mawazo.

Mtaalamu wa maradhi ya kiakili aliiambia mahakama kuwa Pistorius anaugua msongo wa mawazo na anawasiwasi mkubwa baada ya mahakama ya juu zaidi nchini humo kumuongezea makali ya makosa yake, ambapo ilidai kwamba mahakama ya chini ilikosea na hivyo mwanariadha huyo alistahili kujibu mashtaka ya mauaji.

Juni 15, 2016

Pistorius alifiki mahakamani bila ya miguu yake ya bandia, wakati wa kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi ya mauaji yanayomkabili.

Mwanariadha huyo alisimama kizimbani kwa mikongojo, akiinamisha kichwa chake, huku wakili wake Barry Roux, akirejelea kilichotukia usiku wa mauwaji ya mpenziwe Reeva Steenkamp, miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo wanasheria wa mwanariadha huyo walimwambia atembee akiwa hana miguu yake bandia kwa maana ya kumuonesha Jaji ili awe na huruma juu ya ulemavu wake.

Julai 6, 2016

Hii ilikuwa ni siku ya mwisho ya mwanariadha huyo kusikiliza kesi yake, kwa kuwa mahakama ilitoa hukumu kutokana na kosa lake ambapo mwanariadha huyo alihukumiwa kwenda jela miaka sita na tayari ameanza kulitumikia gereza ikiwa leo ni siku ya tano tangu hukumu hiyo itolewe.

Hata hivyo familia ya marehemu Reeva Steenkamp imeonekana kutoridhika na hukumu hiyo huku wakidai kwamba walitamani kuona mwanariadha huyo akienda jela kwa zaidi ya miaka 15 na sio sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles