30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

RUWASA Kagera kutekeleza miradi ya maji kwenye vijiji 19

Na Renatha Kipaka, Bukoba

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) mkoani Kagera inaendelea kutekeleza miradi ya maji kwenye vijiji 19 vyenye wanufaika 127,827 kwa bajeti ya mwaka 2022/2023 ili kufikisha huduma kwa Wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge akikabidhi pikipiki kwa Katibu wa Kamati ya Maji Kemondo mkoani Kagera.

Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Meneja wa RUWASA, Mhandisi Patrice Jerome wakati akitoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa maji kwa mwaka 2021/2022 na miradi inayoendelea kutekelezwa 2022/2023.

Jerome amesema, katika kuongeza kasi ya utendaji na kufikia lengo la Serikali kama sehemu ya mpango wa maendeleo kwa Wananchi Mkoa umefanya na kufikia asilimia 70 ya upatikanaji wa maji safi na salama vijiji.

Amesema licha ya kuwa na tatizo la miradi kuendelea kutekelezwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na sababu mbalimbali bado wakala inaongeza jitihada kwa kila Wilaya ili kufikia maeneo yote yanayokaliwa na Wananchi.

“Kuna tatizo la miradi ya kukamilika zaidi ya mwaka mmoja kulingana na gharama kuwa kubwa kuliko uhalisia wa bajeti iliyopangwa mfano miradi ya fedha za maendeleo ya ustawi wa jamii (Uviko-19) inakuwa na upungufu wa kutosheleza maeneo ya utekelezaji ndanai ya wilaya,” amesema Mhandisi Jerome.

Hata hivyo, kwa mwaka 2021/2022 kulikuwa na miradi 33 inayotekelezwa kutoka vyanzo mbalimbali vya fedha na saba miradi ya maendeleo ya ustawi wa jamii Uviko-19 kwenye vituo 105

Aidha, amesema kwa mwaka 2021/2022 RUWASA iliidhinishishiwa garama ya Sh bilioni 22.1 kutoka mfuko wa maji wa Taifa (NWIF) lipa kwa matokeo (PbR) program ya matokeo (PfrR) fedha ya mfuko wa maendeleo na ustawi wa jamii (Uviko-19) na Ruzuku(GOT).

Nitumie nafasi hii kusema kuwa kwa vyanzo vyote kunakuwa na kiasi kilichotengwa amabacho ni Sh bilioni 25.3 lakini hadi Juni, mwaka huu kiasi kilichopokelewa ni Sh bilioni 24.5,” amesema Mhandisi Jerome

Mhandisi Shukrani Tungaraza kutoka wilayani Kyerwa mbali na usimamizi wa miradi zipo jitihada kuhakikisha wanapata huduma za maji hadi majumbani.

Siyo tu kuweka miradi tunatoa vipaumbele kwa watumia maji ambao ni wananchi kufikisha kwenye majumba yao kwa kufunga bomba na wao kulipia ankara.

Amesema njia hiyo ya maji itasaidia wakusanyaji wa fedha za ankara ya maji zitakazo hudumia ukarabati wa miundombinu inayochakaa au kuharibika.

Awali, akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge amesema serikali inamapango wa kuona miradi inakuwa endelevu na imara kumnufaisha mwananchi.

Ameongeza kuwa mbali na kuwepo muda mwingi ukamilishaji wa miradi, baadhi ya matatizo yameweza kutatuliwa na wizara kwa kutoa usafiri wa pikipiki 12 kwa mkoa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles