29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yamwaga vifaa vya ujenzi vya Milioni 120, Kilimanjaro, Singida na Mbeya

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katika kuhakikisha inaunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za jamii kwa wananchi wake, Benki ya NMB imetoa vifaa mbalimbali katika shule za msingi, Sekondari vyenye thamani ya Sh milioni 120 katika mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro na Singida.

Spika wa Bunge la Jamhuri, Dk.Tulia akipokea msaada wa mabati kati ya mabati 600 yaliyotolewa na Benki ya NMB wakati wa hafla fupi ya makabidhiano katika shule ya Sekondari Iduda,wengine katika picha ni Meya wa Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa, Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara Filbert Mponzi na Meneja wa NMB Kanda Nyanda za Juu Straton Chilongola.

Vifaa hivyo vimetolewa kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo katika mkoa wa Mbeya Benki hiyo ilitoa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 70 hafla ambayo ilihudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Tulia Ackson.

Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Filbert Mponzi wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa shule za Sekondari za Itgano, Itende na Iduda yenye kidato cha tano na sita pamoja na za Msingi Inyala na Ikuti za jijini Mbeya.

Alisema kuwa  Benki hiyo imetoa vifaa kwenye shule hizo ambavyo ni Mabati 200 na madawati 100 kwa kila shule vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh 70 milioni.

Alisema kuwa Benki ya NMB itaendelea kushirikiana na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini ili kuwasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson alipongeza  NMB kwa mchango wake katika sekta ya elimu huku akieleza kuwa  msaada huo utaenda kumaliza tatizo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Iduda.

 “Tunazo shule tano ambazo zitanufaika na msaada huu, tunaamini lile bweni la wasichana hapa Iduda linaenda kuezekwa, wanafunzi nao wakisoma kwenye madawati mazuri,” amesema Dk Tulia.

Mkoani Singida Benki hiyo ilitoa vitanda 80 kwa ajili ya wanafunzi wa bweni  shule za Sekondari Tumaini  na Lulumba zote za Wilayani Iramba pamoja na madawati 100 kwa shule za msingi Ipuli na Ikungu   zote za halmashauri wa Wilaya Mkalama.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alisema kuwa vifaa hivyo vimegharimu kiasi cha Sh milioni 31 huku akibainisha kuwa vitanda vilivyotolewa vitakuwa na uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 160 huku kila shule ikiwa pata madawati 50.

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akipokea msaada wa madawati 400 kwa ajili ya shule 5 za Jiji la Mbeya kutoka kwa Afisa Mkuu wa ateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB Filbert Mponzi, makabidhiano yamefanyika katika shule ya Sekondari Iduda Jijini Mbeya.

Nsolo alisema msaada huo  uliotolwa na Nmb unatokana na faida iliyoipata kwa hiyo wanarudisha  kwenye jamii  sehemu ya faida hiyo kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya maeneo nchini.

Mkuu wa Wiliya ya Iramba, Selemani Mwenda akizungumza baada ya kupokea msaada wa vitanda kwa ajili ya shule hizo mbili aliwashukuru NMB  kwa msaada huo na kuahidi kuwa utakuwa chachu ya shule hizo kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao.

“Shule yetu hii ya Lulumba imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya Kitaifa na imekuwa ikiongoza kwa matokeo katika Mkoa wetu kwa kushika nafasi ya kwanza  na imekuwa  ikishika nafasi ya juu Kitaifa  hivyo vitanda hivi tulivyokabidhiwa leo itakuwa chachu ya kufanya vizuri zaidi”alisema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ,Sophia  Kizigo akashukuru NMB kwa msaada wa madawati, huku akizuomba taasisi nyingine kuiga mfano wa benki hiyo katika kuunga mkono juhudi za serikali kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Mkoani Kilimanjaro Benki hiyi imetoa viti pamoja na Meza 200 kwa shule ya Sekondari Kivisini iliyopo katika Wilaya ya Mwanga, ambapo vifaa hivyo vilipokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Abdala Mwaipaya.

Meneja wa NMB Kanda a Kaskazini Dismas Prosper akikabidhi viti na meza hivyo alisema kuwa vimegharimu kiasi cha Sh. Milioni 20.8 na kubainisha kuwa lengo la kutolewa kwa vifaa hivyo ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles