29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

RUTO: SHAMBULIO DHIDI YA NGUMBA YANGU LILILENGA KULETA WASIWASI

ELDORET, KENYA

NAIBU Rais William Ruto amesema shambulio dhidi ya makazi yake ya Sugoi yalilenga kuvuruga umoja miongoni mwa Wakenya.

Akizungumza kwa waumini kwenye uwanja wa Ihura huko Murang’a, naibu rais aliwataka Wakenya kubakia wamoja na watulivu.

“Najua watu wengi walifahamu nilikuwa na wageni wengi jana(juzi) lakini nataka kusema wale waliodhani watatikisa umoja wetu au kukwamisha maendeleo yetu, hawatafanikiwa,” alisema hayo wakati wa kusimikwa kwa Askofu Timothy Gichere kuwa Mkuu wa Dayosisi ya Mlima Kenya Kati.

“Nataka kuwaambia sisi sote hatuwezi kutishwa na njama za watu wanaolenga kuvuruga umoja wetu na maendeleo ya taifa letu,” alisema.

Jumamosi, Inspekta Jenerali wa Polisi Joseph Boinnet alisema mtu asiyejulikana alimshambulia askari wa polisi aliyekuwa akilinda getini na kuingia ndani kisha kuchukua silaha.

Kufuatia tukio hilo, kikosi cha polisi cha Recce kiliizingira nyumba hiyo kwa saa 20 kumwondoa mtu huyo.

Jana asubuhi, Mratibu wa Eneo la Rift Valley Wanyama Musiambo alisema waliothirika katika operesheni hiyo ni pamoja na mshambuliaji ambaye aliyuawa na maofisa wawili wa polisi.

Mtu huyo alimuua ofisa mmoja na kumjeruhi mwingine ambaye anapata matibabu hospitali.

“Mtuhuyo alikuwa akitumia silaha tofauti ili kuwachanganya maofisa wa polisi kuwa wako wengi,” Musiambo alisema akiongeza kuwa usalama umerudishwa katika makazi hayo.

Wakati wa shambulio katika makazi hayo yaliyopo Kaunti ya Uasin Gishu, Ruto alikuwa akiendesha kampeni katika Kaunti ya Kitale baada ya kuondoka hapo asubuhi siku hiyo na familia yake haikuwapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles