26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

RUSHWA YAMPELEKA JELA ‘MRITHI’ SAMSUNG

SEOUL, KOREA KUSINI

MAHAKAMA nchini Korea Kusini imemhukumu bilionea anayetarajiwa kurithi kampuni ya Samsung, Lee Jae-yong, kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya utoaji rushwa.

Lee alikuwa ameshtakiwa kuhusika katika rushwa katika kashfa ambayo pia ilichangia kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Korea Kusini.

Kesi hiyo ilikuwa imevutia sana umma huku hasira zikiendelea kupanda dhidi ya kampuni kubwa za kibiashara za Korea Kaskazini maarufu kama chaebols.

Lee ambaye amekanusha mashtaka yote, alikuwa amekabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela hadi miaka 12.

Aidha, Lee anafahamika kama Jay Y Lee na amekuwa ndiye kiongozi wa kampuni hiyo kubwa zaidi ya kutengeza simu duniani, amekuwa kizuizini tangu Februari mwaka huu akikabiliwa na tuhuma kadhaa za rushwa.

Miongoni mwa makosa aliyokabiliwa nayo ni utoaji rushwa, wizi wa mali ya umma na kuficha mali nje ya nchi.

Pia alituhumiwa kutoa mchango wa hisani wa dola milioni 36 kwa nyakfu za hisani zilizosimamiwa na rafiki wa karibu wa rais aliyeondolewa madarakani Park Geun-hye, ndipo apendelewe kisiasa.

Waendesha mashtaka wanasema mchango huo ulitolewa kwa mwandani mkuu wa Rais Park, ili Serikali iunge mkono mageuzi katika mfumo wa usimamizi wa kampuni ya Samsung ambao ungempatia Lee nguvu zaidi katika udhibiti wa kampuni ya Samsung Electronics.

Wakili wa Lee amesema tayari kwamba watakata rufaa uamuzi huo.

“Tuna imani kwamba hukumu hii itabatilishwa,” wakili Song Wu-cheol ameambia wanahabari baada ya kusomwa kwa hukumu, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters.

Hata hivyo, uamuzi huo wa mahakama ni pigo kubwa kwa kampuni hiyo kubwa zaidi na inayofahamika zaidi ya Korea Kusini.

Hukumu hiyo imetilia shaka sasa uongozi wa Lee katika kampuni hiyo.

Amekuwa kaimu mwenyekiti tangu baba yake Lee Kun-hee alipopatwa na mshtuko wa moyo mwaka 2014. Kashfa hiyo ya Samsung ilichangia kuondolewa madarakani kwa Rais Park. Mwandani wake Choi Soon-sil tayari amefungwa jela miaka mitatu kwa makosa ya rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles