24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

RUFAA YA WASIRA KUANZA KESHO

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania imepanga kusikiliza rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Bunda kesho.  

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo jana katika rufaa iliyokatwa na wapigakura wanne wa jimbo hilo baada jopo la majaji watatu kukwama kuanza kusikiliza kwa sababu  ya makosa yaliyofanyika kwa vile Wakili wa Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya, Tundu Lissu hakuipata notisi ya kuitwa mahakamani.

Jopo la majaji linaloongozwa na  Jaji Mbarouk Mbarouk liliahirisha usikilizwaji huo hadi kesho na kuamuru makosa hayo yasirudiwe tena kwa kuwa yamewapotezea muda na wana mambo mengi ya kufanya.

Warufani wanawakilishwa na mawakili Yassin Member na Constantine Mutalemwa huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiwakilishwa na mMawakili wa serikali, Obadia Kamea na Angela Msagala.

Wakili wa mjibu rufani wa kwanza ambaye Bulaya, Lissu hakuwapo mahakamani hivyo  mawakili wa wakata rufaa waliomba kesi iahirishwe kwa muda mfupi kutokana na umuhimu wake.

Jopo hilo, Jaji Mbarouk, Augustino Mwarija na Rehema Mkuye, lilikubaliana na ombi hilo, hivyo kuamua kuahirisha usikilizwaji huo hadi kesho.

“Inasikitisha, haipendezi mnaopeleka notisi muwe makini kwa sababu mnatupotezea muda wakati tuna mambo mengi ya kufanya, hili kosa lisijirudie tena, sisi tulikuwa tayari kusikiliza na tulipanga kesi moja tu,” alisema Jaji Mbarouk.

Wakata rufaa katika kesi hiyo ya uchaguzi Jimbo la Bunda ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila ambao walikata rufani dhidi ya Bulaya, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Wakili Mutalemwa alitaja sababu za kukata rufani  kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na ukiukwaji wa wazi wa sheria za uchaguzi na kanuni.

Alidai tafsiri isiyo sahihi ya kanuni za uendeshaji kesi za uchaguzi kuhusiana na viapo na kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi kwa kutomtaarifu mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mahali na tarehe ya kujumuisha kura na taarifa ya mwisho ya matokeo kuwa na idadi kubwa ya waliojiandikisha kupiga kura tofauti na Tume ya Uchaguzi ya Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles