23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

RT anzeni na Michezo ya Afrika kabla ya Olimpiki


KWA kipindi kirefu sasa, mchezo wa riadha hapa nchini umeendelea kuwa taabani.

Umekuwa utamaduni wa kawaida kwa wanariadha wetu kurejea nchini mikono mitupu pale wanaposhiriki mashindano ya kimataifa.

Yapo mengi yamekuwa yakitajwa kuwa sababu ya mchezo huo kuwa kwenye hali mbaya, ikiwamo maandalizi duni ambayo hufanywa na wanariadha kabla ya kushiriki mashindano ya kimataifa.

Mara nyingi wanariadha wa Tanzania wamekuwa na maandalizi ya kulipua, yasiyoendana na ushindani uliopo kwenye mashindano ya kimataifa.

MTANZANIA pamoja na wadau wengi wa michezo kiu yetu ni kuliona Shirikisho la Riadha Tanzania(RT), likiufufua mchezo huo ambao miaka ya nyumba ulilitelea sifa na kuitangaza vyema taifa letu nje ya mipaka yake.

Hata hivyo, yapo maswali ya kujiuliza, baada ya kusikika kwa kauli ya Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday, ambaye hivi karibuni alisema  watahakikisha wanariadha wa Tanzania wanarudi na medali katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani, Tokyo nchini Japan.

Ni wazo zuri, hasa ikizingatiwa kuwa, wadau wa riadha hapa nchini wamechoshwa na utamaduni wa wanamichezo wao kuwa wasindikizaji kwenye mashindano ya kimataifa.

Hata hivyo, ikiwa imebaki takribani miezi michache kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, hali ya mchezo wa riadha bado hairidhishi kiasi cha kuanza kuziota medali.

Hatukatai tunaweza kuambulia medali, lakini hofu yetu inaweza ikapatikana kwa kubahatisha na si kutokana na mipango thabiti ya RT.

Kwa tathmini ya haraka, inaweza kutuchukua hata zaidi ya miaka 10 na kuufanya mchezo wa riadha kufikia anga za majirani zetu Kenya, Ethiopia na Jamaica, si jambo la kipindi kifupi.

Bado changamoto za mchezo wa riadha ni nyingi mno na zinatakiwa kutolewa macho na si kuanza kuziweka akilini medali za Tokyo.

Kwa sasa, riadha si miongoni mwa michezo inayopewa nafasi kubwa katika shule zetu, mwamko ni mdogo katika ngazi za chini, pia viwanja vyenye ubora wa kimataifa ni tatizo sugu.

Kama changamoto hizo zitafanyiwa kazi, basi mchezo wa riadha hapa nchini utakuwa umepiga hatua kuliko kushinda medali 10 za Tokyo bila mipango thabiti.

Pia, kutokana na uwepo wa miundombinu inayosapoti maendeleo ya mchezo huo, kutakuwa na mwendelezo wa mafanikio ya wanamichezo wetu kwenye michuano ya kimataifa.

Kama Tanzania itafanikiwa kunyakua medali mwakani ikiwa na kasoro hizo, hilo halitatugfanya tuwe na imani ya kuvuna nyingine mwaka 2024.

Tutabaki kutegemea bahati na si mipango thabiti inayoweza kutumiwa na mwanariadha mwingine yeyote wa Tanzania kushinda medali.

Kwa upande mwingine, RT kabla hawajafikiria mipango hiyo ya Olimpiki wanatakiwa kupigania maandalizi ya mashindano ya kimataifa yalio mbele, ili Watanzania waweze kuwa na imani na wanariadha wao.

Watanzania wengi wana hamu ya kuona medali zinapatikana kwamba katika mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika Septemba, kisha ‘All Africans Games’(Michezo ya Afrika) ambayo itakayofanyika Agosti.

Tunafahamu mashindano hayo ni makubwa na yana ushindani, hivyo RT inatakiwa kutafuta namna ya| kuwasaidia wanaridha ili waweze kuvuna medali katika mashindano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles