Walter Mguluchuma, Katavi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amewaagiza Askari Polisi wa mkoani hapa, kuhakikisha wanawapigia saluti wabunge wanapokuwa kwenye majimbo yao kama maelekezo ya jeshi hilo yanavyoelekeza.
Kamanda Nyanda alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na polisi wa ngazi mbalimbali wa mkoa huo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa fenicha zikiwamo meza na viti vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (CCM), kwa ajili ya Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda.
“Ni vizuri mkatambua nafasi za waheshiwa wabunge kwani wapo baadhi ya askari hata wanapokuwa wanakutana na wabunge wamekuwa hawajali nafasi zao na wamekuwa hawawapigii saluti.
“GPO namba 102 ya Jeshi la Polisi inaekekeza ni viongozi wapi wanaotakiwa kupigiwa saluti wakiwamo na wabunge lakini askari polisi wamekuwa baadhi yao hawapigii saluti wabunge wao, hivyo watambue kuwa wanafanya makosa, suala hili si hiari ni lazima,” amesema.