22.5 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Rooney: Sina mpango wa kuiacha England

Wayne Rooney
Wayne Rooney

PARIS, UFARANSA

BAADA ya timu ya Taifa ya England kutolewa katika michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa, nahodha wa timu hiyo, Wayne Rooney, amedai kwamba hana mpango wa kujiuzulu kuitumikia timu hiyo.

England imetolewa katika hatua ya 16 bora dhidi ya wapinzani wao Iceland kwa mabao 2-1, hivyo kumfanya kocha wa timu hiyo, Roy Hodgson, kujiuzulu kutokana na kichapo hicho, ila Rooney amesema hawezi kujiuzulu.

“Ni kweli ninajisikia vibaya kuona tunatolewa katika hatua hii ya 16 bora, niliamini kuwa tulikuwa na kikosi kizuri ambacho kingeweza kufika mbali na hata kutwaa ubingwa, lakini hali imekuwa tofauti na tumetolewa.

“Kocha wetu ametangaza kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya, lakini kwa upande wangu sina mpango huo wa kufanya kama alivyofanya Hodgson, natarajia kuona kocha mpya akijiunga na sisi katika michuano mingine, ninaamini nitakuja kujifunza kitu kutoka kwake.

“Wachezaji wote tumeumia na matokeo hayo lakini tunatakiwa kukubaliana nayo na tujipange kwa ajili ya michuano mingine ili tuweze kuwakilisha taifa letu,” alisema Rooney

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles