27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

ROONEY AWEKA REKODI YA MABAO ENGLAND

LONDON, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Everton, Wayne Rooney, ameingia kwenye historia mpya ya kufikisha jumla ya mabao 200 katika michuano ya Ligi Kuu nchini England, ikiwa ni mchezaji wa pili kufikisha idadi kubwa ya mabao kwenye ligi.

Mshambuliaji huyo juzi aliisaidia timu yake hiyo kupachika bao kwenye mchezo dhidi ya Manchester City, huku ukimalizika kwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Etihad.

Rooney ameingia kwenye historia hiyo mpya ya kuwa mchezaji wa pili katika Ligi ya England kuwa na mabao mengi, anaungana na Alan Shearer ambaye ni kinara wa mabao akiwa na jumla ya 283.

Nahodha huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United, bao la juzi lilikuwa la pili katika ligi tangu ajiunge na Everton katika kipindi hiki cha majira ya joto akitokea Manchester United.

Mchezaji huyo akiwa katika klabu ya Manchester United, alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 183 wakati huo akiwa ndani ya Everton kabla ya kujiunga na Man United mwaka 2004, alifunga jumla ya mabao 15 katika michezo 67 aliyocheza na sasa amefunga mabao mawili tangu ajiunge msimu huu hivyo kuwa na jumla ya mabao 200.

Wakati huo Shearer alifanikiwa kufikia idadi hiyo kubwa ya mabao tangu msimu wa mwaka 1992-93 katika Ligi Kuu nchini England na hadi sasa bado mchezaji huyo anaongoza kwa kuwa na mabao mengi katika ligi hiyo.

Shearer alifikisha mabao hayo baada ya kucheza katika klabu ya Southampton na kufunga mabao 23, Blackburn Rovers akifunga mabao 112 na Newcastle United akifunga mabao 148 na kuwa jumla ya mabao 283.

Shearer alitumia ukurasa wake wa Twitter kumpongeza Rooney kwa kufikisha mabao 200 na kumtaka ajitume ili aweze kuwa na idadi kubwa zaidi.

“Nimekuwa peke yangu kwa kipindi kirefu kwenye historia hii ya mabao mengi, hongera sana kwa kufikisha mabao 200. Karibu sana na endelea kujituma ili kuwa na idadi kubwa katika historia hiyo,” alisema Shearer.

Baadhi ya wachezaji wengine ambao wana mabao mengi ni pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Andy Cole, akiwa na mabao 187, Frank Lampard akiwa na mabao 177, wakati huo Jermain Defoe akiwa na mabao 158 na Sergio Aguero akiwa na 123, Defoe na Aguero ni miongoni mwa wachezaji wanaoendelea kucheza soka hadi sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles