27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

GATLIN AWAOMBA RADHI MASHABIKI

NEW YORK, MAREKANI

BINGWA wa riadha wa mbio za mita 100 kwenye mashindano ya dunia nchini England mwaka huu, Justin Gatlin, amewaomba radhi mashabiki kwa kutumia dawa zisizokubalika michezoni.

Nyota huyo raia wa nchini Marekani alikutwa na kashfa hiyo katika mashindano ya mwaka 2004 na 2006, hivyo mwaka huu alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushinda mbio hizo na mashabiki kuamua kumzomea.

Gatlin amethibitisha kwamba alikosa furaha japokuwa aliweza kuwa bingwa mbele ya mpinzani wake, Usain Bolt, kutokana na mashabiki kumzomea.

Baadhi ya mashabiki walitumia mitandao ya kijamii na kumshambulia bingwa huyo huku wakidai kwamba inawezekana atakuwa amedanganya tena kwenye mbio za mwaka huu kwa kutumia dawa za kusisimua misuli.

“Nilijisikia vibaya sana kuzomewa na mashabiki wakati huo nachukua ubingwa, pale sikuwa kwa ajili yangu binafsi, ila nilikuwa kwa ajili ya kuliwakilisha taifa na kuwapa furaja mashabiki.

“Nilisikia kelele za kunizomea, nilijisikia vibaya sana kwa kuwa nilikuwa pale kwa ajili ya taifa na mashabiki wanaoipenda nchi yao.  

“Nadhani wale walionizomea wengi wao hawakuwepo kwenye michuano ya 2004 na 2006, lakini wamekuwa na chuki na mimi kutokana na kile kilichotokea kipindi hicho, hivyo wapo kwenye historia.

“Nadhani wanataka nisimame mbele yao na kuwaomba radhi, napenda kutumia nafasi hii kusema samahani kwa kile kilichotokea miaka hiyo iliyopita, bado ninapenda sana riadha na ndio maana nikarudi tena kwenye mchezo huu na kufanya makubwa zaidi, nilifanya hivyo ili kujaribu kuwashawishi mashabiki kwamba sikuwa muongo,” alisema Gatlin.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles