26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Riyama: Maneno machafu yananipa chakula

Riyama-AliNA GEORGE KAYALA
MSANII mwenye heshima kubwa kwenye tasnia ya filamu za Bongo, Riyama Ally, ameibuka na kujivunia kwamba maneno machafu anayoyatumia katika filamu mbalimbali anazocheza ndiyo yanayompa chakula cha kila siku.
Riyama alisema katika filamu mbalimbali alizocheza amekuwa akitumia maneno ya kashfa, kejeli ambayo yameonyesha kuvutia waongozaji wengi wa filamu nchini kumtumia katika filamu zao.
“Nina kila sababu ya kujivunia maneno machafu ya uswahilini kwani hayo ndiyo yananifanya nipate mialiko mingi ya kuigiza kama nilivyoshirikishwa kwenye filamu mbalimbali na sasa naheshimika kwa maneno hayo ingawa wapo baadhi wanafikiri ndiyo maisha yangu halisi wakati naigiza,” alijieleza Riyama ambaye kwa sasa anatamba katika filamu ya Uwoga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles