Inspekta Haroon: Nataka kuwa mchekeshaji

0
1019

INSPECTOR.Na Rhobi Chacha
UNALIKUMBUKA kundi la Gangwe Mobb, hapo lazima utamtaja Haruna Kaena ‘Insepkta Haroun’ na Luten Kalama, wawili hao baada ya kutengana kila mmoja akawa anafanya kazi binafsi lakini sasa Inspekta Haroun ameibuka na kudai kwamba anataka kuwa mwigizaji wa vichekesho.
Inspekta Haroun aliyetamba na wimbo wa ‘Mtoto wa Geti Kali’ aliendelea kueleza kwamba fani anazozipenda ni muziki na kuigiza vichekesho.
“Mimi msanii hivyo natakiwa niwe mbunifu, nisibweteke na kazi, fani moja na kwa sasa napenda kuwa mwigizaji wa vichekesho kwa kuwa napenda kazi hiyo na ninaiweza,” alijinadi.
Msanii huyo aliwahi kushirikishwa katika vipengele vya uigizaji katika kipindi cha vichekesho kilichokuwa kikirushwa na televisheni ya Clouds.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here