30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

RIPOTI YA OBG KULETA FURSA UKUAJI UCHUMI TANZANIA

Na GEORGE MSHANA


[ 

WAKATI Afrika inaonekana ni sehemu nzuri ya uwekezaji, ni wakati mzuri pia kwa Tanzania kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo kwenye vyombo vya habari vya kimataifa na kuboresha mazingira ya kufanya biashara ili kuvutia wawekezaji kuwekeza hapa nchini na hatimaye kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, katika utiaji saini wa makubaliano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Oxford Business Group (OBG) kwa ajili ya utafiti wa kimataifa na taasisi ya kutoa ushauri wakati wakizindua ripoti juu ya uchumi wa nchi.

Chini ya makubaliano hayo, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kitasaidia katika utafiti kwa timu ya OBG na imeanza kukusanya takwimu kwa ajili ya ripoti hiyo. Ripoti hiyo ambayo itakuwa na kurasa 200 zenye uchambuzi juu ya mazingira ya uwekezaji na ya biashara ya Tanzania, itachapishwa mwaka huu.

Ushirikiano huu wa utafiti ulisainiwa hivi karibuni katika ofisi za Kituo cha Uwekezaji (TIC) na Waziri Charles Mwijage na Clifford Tandari, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji walikuwepo. Wazungumzaji wote walitoa mawazo yao kuhusiana na mazingira ya uwekezaji ya Tanzania na pia walizungumzia umuhimu wa kuhakikisha kwamba wawekezaji wanaweza kupata ushauri wa kibiashara kutoka kwa wataalamu wetu wa uchumi na biashara.

Ripoti hiyo itaangalia kwa undani fursa na changamoto wanazozipata wawekezaji wa nje hapa nchini Tanzania. OBG wataangalia ukuaji wa uchumi wa Tanzania, hasa baada ya ugunduzi wa gesi asilia na jitihada za Serikali katika kufikia malengo ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Malengo haya yatawafanya wawekezaji wengi wanaokuja kuwekeza Tanzania kuelimishwa kuhusiana na fursa zilizopo katika sekta ya viwanda na hivyo kuamua kuwekeza katika sekta hiyo.

Akiikaribisha OBG nchini Tanzania, Mwijage alisema ana imani ripoti hiyo itaifanya OBG iwe na wasifu  wa juu kati ya wawekezaji wa kimataifa.

“Tunatambua umuhimu wa kutengeneza mazingira ya kuvutia kwa wawekezaji wa nje na kuhakikisha kwamba wanapata taarifa kuhusiana na fursa zilizopo za uwekezaji hapa nchini. Oxford Business Group inaheshimika na kutambulika kwa kufanya utafiti wa kina wa kiuchumi. Natarajia kutokana na kazi iliyofanywa na wataalamu wake na Kituo cha Uwekezaji, wataona fursa za maendeleo katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa,” alisema Waziri Mwijage.

Naye kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Tandari, amesema anakubali kwamba ripoti ya OBG itakuwa na mchango mkubwa kwa wasomaji wa ripoti hiyo kwa kuwapa habari muhimu za ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Wakati siku za nyuma tulikuwa tunategemea mikutano ili kuwaeleza wawekezaji juu ya fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania, ripoti ya OBG itakuwa kama njia muhimu ya kuwasilisha takwimu na uchambuzi wa masuala ya uchumi na kuziweka kwenye mtandao wa kimataifa na kuchapisha kwenye karatasi, kidijitali na kwa njia ya video na kuzisambaza duniani kote ili watu wasome fursa za kiuchumi na kiuwekezaji zilizopo hapa nchini Tanzania na hivyo kuja kuwekeza Tanzania na kuifanya uchumi wake ukue na nafasi za ajira kuongezeka pia.  

Mkurugenzi wa OBG Tanzania, Ivana Carapic, amesema anatarajia kufanya kazi na timu ya Kituo cha Uwekezaji katika mradi huu ambao utakuwa na manufaa sana kwa uchumi wa Tanzania.

“Pamoja na kuanzia chini, Tanzania ipo katika nafasi nzuri kwa kutimiza lengo lake la kuwa nchi ya uchumi wa kati mwaka 2025, ikiwa imezipita nchi jirani kwa kuwa na uchumi imara katika miaka ya hivi karibuni,” alisema Carapic.

Ripoti hii itakuwa ya muhimu sana kwa nchi yetu, ikiwa ni pamoja na uchumi mkuu, miundombinu na sekta ya benki. Ripoti hii pia itajumuisha mahojiano na wawakilishi wa nchi. Itakuwepo kwenye makaratasi (hard copy) na kwenye mtandao. Watu wengi sana duniani kote wanatarajiwa kuisoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles