26.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 4, 2024

Contact us: [email protected]

Ripoti ya Lugumi yakabidhiwa kwa Spika

Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spika wa Bunge, Job Ndugai

Na SARAH MOSES, DODOMA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali mstaafu Projestus Rwegasira, amekabidhi ripoti ya vifaa vya utambuzi wa alama za vidole katika vituo vya polisi vya wilaya 108 nchini kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Ripoti hiyo inatokana na maelekezo yaliyotolewa na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson aliyoyatoa bungeni Juni 30, mwaka huu kwa kuiagiza Serikali ihakikishe inafunga mashine hizo kwa kipindi cha miezi mitatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghejwa Kaboyoka alisema ripoti hiyo imekabidhiwa kwa Spika wa Bunge, ambaye ataikabidhi kwa kamati yake kwa hatua zaidi.

Hatua ya kukabidhiwa kwa ripoti hiyo kumetokana na mkataba tata ulioingiwa kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited wenye thamani ya Sh bilioni 37.

Mkataba huo ulisainiwa mwaka 2011 ukiwa na lengo la kufunga mashine hizo za utambuzi katika vituo vya polisi 108 nchini lakini hadi wakati huo ni vituo 10 tu ndivyo vilivyokuwa na mashine hizo.

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2013/14  ilionyesha kuwa pamoja na Kampuni ya Lugumi kulipwa asilimia 99 ya malipo sawa na Sh bilioni 34, bado haijakamilisha mradi huo kwa muda wa miaka mitano sasa.

Aprili mwaka huu Kamati ya PAC iliunda kamati ndogo kwa ajili ya kuchunguza mkataba huo wa utata baina ya Kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga (CCM).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles