25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ripoti Transparency: Vijana Afrika wahusishwa kutoa rushwa zaidi

SHIRIKA  la kukabiliana na ufisadi la kimataifa la Transparency International  limetoa ripoti inayoonyesha vijana wa Afrika wenye umri wa kati ya miaka 18-34, wana uwezekano mkubwa wa kutoa rushwa kuliko watu wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 55.

Katika kipimo chake cha kiwango cha ufisadi duniani cha mwaka 2019, shirika hilo limesema utafiti wake pia umebaini watu maskini zaidi wana uwezekano mara mbili zaidi wa kutoa rushwa – na wana uwezekano mkubwa pia wa kuwa waathiriwa wa rushwa inayosababishwa na tabia ya urasimu kuliko matajiri.

Utafiti huo wa kila mwaka ambao kwa mwaka huu ni wa 10, katika bara la Afrika umeitaja  nchi ya Jamuhuri ya Kongo kuwa ndiyo yenye  kiwango cha juu zaidi ikiwa na asilimia 75  ya wale waliotoa hongo kwa polisi.

Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa raia wa kigeni pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuchochea na kushiriki vitendo vya rushwa katika bara la Afrika.

Kwa sababu hiyo wametajwa kuhujumu maendeleo ya kudumu ya kikanda.

Transparency International linasema kuwa kampuni za kigeni hutoa hongo ili kupata mikataba kama vile ya haki ya uchimbaji wa madini, mikataba ya ujenzi wa miradi mikubwa na mikataba mingine.

Transparency International linasema pia kwamba matokeo ya utafiti wake yametokana na mahojiano ya ana kwa ana kati ya Septemba 2016 na Septemba 2018, yaliyofanyika kwa ushirikiano na taasisi ya utafiti wa kimaendeleo barani Afrika-Afrobarometer.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles