24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 29, 2023

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti wa zamani wa UWT kizimbani kwa kughusi cheti cha ndoa

ERICK MUGISHA (DSJ) – DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Ilala Norah Waziri (52), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa shtaka la  kughushi cheti cha ndoa.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Benson Mwaitenda, akimsomea shtaka lake mbele ya Hakimu, Anifa Mwingira, alidai Februari 4 mwaka 1995 jijini  Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya mtuhumiwa alighushi cheti cha ndoa chenye namba za usajili 00040078  kikionyesha ameolewa na Silvanus Mzeru katika Kanisa Katoliki la Mburahati.

Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo mwendesha mashitaka alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hakimu Mwingira alisema dhamana ipo wazi kwa mashariti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua zinazo watambulisha wanapotokea, vitambulisho vya Taifa na kusaini bondi ya Sh milioni moja.

Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza mashariti na kesi hiyo itatajwa tena Julai 17.

Wakati huo huo watu wawili amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa shtaka la mauaji.

Waliofikishwa Mahakamani ni Juma Malumbi (34) mkazi wa Kinondoni Hananasif na Amri Mazangu (40) mkazi wa Mbagala Kirulugwa.

akiwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, ASP Hamisi, alidai Octoba 20 mwaka 2018 maeneo ya Bonde la Mchicha Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam, watuhumiwa walimuua Zurufa Oda.

Hakimu Mushi alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

ASP Hamisi alidai upelelezi hauja kamilika na kuomba tarehe nyingine kwa kesi hiyo kutajwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,259FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles