29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

RIPOTI KAMATI YA ADADI HAIJAKAMILIKA

Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama imeshindwa kuwasilisha bungeni ripoti yake bungeni leo kutokana na kutokamilisha kazi yake.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Adadi Rajabu amesema kamati inaendelea na kazi hiyo na itawasilisha ripoti yake baada ya kukamilika bila kutaja siku.

Hoja ya kamati hiyo kukutana na vyombo vya ulinzi na usalama, iliyopitishwa na Bunge wiki iliyopita baada ya Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), kutoa pendekezo hilo, ambapo jana Spika wa Bunge, Job Ndugai alitoa taarifa kuwa kamati hiyo ingetoa ripoti yake leo kabla ya kuahirishwa kwa shughuli za Bunge.

Katika hoja yake, Bashe alitumia kanuni ya 47, sehemu ya kwanza na ya pili akirejea tukio la kushambuliwa kwa risasi, Mbunge Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema).

Akitoa majibu ya hoja hiyo, Spika Ndugai alisema hana tatizo juu ya kamati hiyo ya Bunge kukutana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuwa hoja hiyo ni ya msingi ambapo alimtaka Mwenyekiti wa kamati hiyo kukutana na wajumbe wake na kuleta taarifa kabla ya kuahirishwa kwa bunge leo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles