30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Rihanna akera mashabiki California

RihannaCALIFORNIA, MAREKANI

NYOTA wa muziki wa Pop na RnB nchini Marekani, Robyn Rihanna, amewaacha njiapanda mashabiki wake jijini California katika tamasha la SAP Center ambalo lilifanyika San Jose jijini California juzi kwa kushindwa kupanda jukwaani.

Mashabiki walijitokeza kwa wingi na kumsubiri msanii huyo, lakini hakutokea kwenye tamasha hilo kwa madai kwamba msafara wake ulipata ajali.

“Najua mashabiki walikuwa wananisubiri sana, lakini kuna mambo yalitokea nje ya uwezo wetu, msafara wangu ulipata ajali hivyo ningeweza kuja lakini ningechelewa na ingekuwa haina maana yoyote.

“Ninawaahidi kuja tena mambo yakiwa sawa kwa ajili ya kuja kulipa fadhila zenu za muda ambao mliutumia na kuja kufurahi pamoja,” aliandika Rihanna kwenye akaunti yake ya Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles