RIHANNA AKANUSHA KUTOKA NA LEROY SANE

0
985

NEW YORK, MAREKANI


MSANII wa muziki wa pop nchini Marekani, Rihanna Fenty, amekanusha taarifa za kwamba yupo kwenye uhusiano na kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Leroy Sane.

Wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii nchini Marekani zilienea picha ambazo zilidaiwa kuwa ni Rihanna na nyota huyo wa soka wakiwa pamoja kimahaba, lakini msanii huyo amekanusha kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Sijashangaa kuona watu wananizungumzia, lakini nimeshangaa kuhusishwa kuwa kwenye uhusiano na Sane, hakuna ukweli wowote na wala sijawahi kuwa karibu na mchezaji huyo kama watu wanavyodhani.

“Picha ambayo ninafananishwa na msichana ambayo yupo na mchezaji huyo nimeiona, lakini niweke wazi kwamba siyo mimi,” alisema Rihanna.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here