26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

HOSPITALI YA MAWENZI YAPIGA MSASA VIJANA.

Na UPENDO MOSHA-MOSHIHOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi, imeanza kutoa elimu ya afya ya uzazi na huduma rafiki kwa vijana wenye umri wa miaka 10
hadi 24.

 

Ofisa Muuguzi katika Hospitali ya Mawenzi, Anna David, alisema jana kwamba, lengo la elimu hiyo ni kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi na mimba za utotoni kwa vijana.

David aliyasema hayo jana wakati akitoa mafunzo kwa vijana wa vituo vya huduma ya mtoto na vijana katika makanisa ya kiinjili, eneo la Moshi mkoani Kilimanjaro.

 

“Tumeona kuna umuhimu wa kuanza mchakato huo wa kutoa elimu kwa watoto na vijana kwa kuwa wengi wao wamejikuta wakipata mimba za utotoni na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

 

“Kundi la vijana limeonekana likisahaulika kwani wazazi hawana muda wa kuzungumza nao na walimu wana muda mchache pia wa kuwa nao.

 

“Kwa hiyo, elimu tunayotoa itakuwa ni huduma rafiki kwa vijana na itakuwa chachu ya kuwanusuru dhidi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba za utotoni,” alisema David.

 

Naye Makamu Mwenyekiti wa Vituo vya Huduma ya Mtoto na Vijana katika Makanisa ya Kiinjili Klasta ya Moshi, Patrick Mugusie, alisema
wamekuwa wakiwahudumia watoto katika mambo makuu manne ambayo ni kiroho, kiafya, kielimu na uraia wema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles