Rhino The Don kuwapa raha mashabiki Januari 8

0
402

Na CHRISTOPHER MSEKENA

STAA wa Bongo Fleva anayefanya muziki nchini Marekani, Rhino The Don, ametangaza neema kwa mashabiki wake kukaa tayari kwa ujio wa ngoma mpya, Tingisha utakaotoka Januari, 8, 2021.

Rhino, ameweka wazi kuwa wimbo huo ni moto zaidi kuliko Wekaa aliyofanya na Shetta na ile Sibanduki Kwake aliyomshirikisha Mr Blue, hivyo mashabiki wakae mkao wa kuburudika.

“Nimefunga mwaka 2020 na ngoma niliyofanya na Mr Blue, nashukuru imekuwa kali sana na watu waliipenda, sasa hivi najiandaa kuachia jiwe lingine nadhani Januari, 8, 2021 kwahiyo watu wakae mkao wa kula bata,” alisema Rhino.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here