24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Remtullah, Hassanali, Kadinda kukinukisha mbugani

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

MANGULI wa mitindo nchini wanatarajiwa kushiriki tamasha la mavazi liitwalo Safari Fashion Weekend litakalofanyika Januari 28 hadi 30, mwaka huu katika Hoteli ya Mawemawe mkoani Manyara.

Wabunifu hao ambao tayari wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni Ally Rehmtullah, Bahati Zanzibar, Cocolili, Doreen Mashika, Jamilla Vera Swai, Martini Kadinda, Mustafa Hasanali na Schwari.

Lengo la tamasha hilo ni kukuza na kutangaza utalii wa ndani kupitia tasnia ya mitindo pia kuonyesha mavazi yanayo valiwa katika safari za utalii.

Kabla ya tamasha hilo ambalo kiingilio kitakuwa ni dola 50 kutakuwa na shughuli za utalii wa ndani ambapo wabunifu watatembelea vivutio vilivyomo ndani ya Hoteli ya Mawe Mawe.

Januari 29, kutakuwa na mnada ambao wabunifu watauza mavazi yao na bidhaa zengine Mawemawe hoteli.

Usahili kwa ajili ya kupata wanamitindo watakaoshiriki tamasha hilo utafanyika Januari 15, mwaka huu katika Ukumbi wa Makuti Restaurant uliopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles