28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Real Madrid kufungiwa kushiriki Copa del Rey

realMADRID, HISPANIA

KLABU ya Real Madrid inawezekana ikafungiwa kushiriki Kombe la Copa del Rey baada ya kumtumia mchezaji wake, Denis Cheryshev, ambaye alikuwa anatakiwa kutumikia kadi tatu za njano ambazo alioneshwa msimu uliopita.

Katika mchezo huo wa juzi, Madrid walifanikiwa kushinda mabao 3-1 dhidi ya Cadiz, huku Cheryshev akipachika bao la kwanza kabla ya Isco kuongeza mabao mawili.

Rais wa klabu ya Cadiz, Manuel Vizcaino, amesisitiza kuwa lazima atoe taarifa kwa chama cha soka nchini Hispania juu ya wapinzani wao, Madrid kumtumia mchezaji huyo ambaye alitakiwa kutumikia kadi.

 

“Tunatakiwa kutoa taarifa kwa chama cha soka juu ya tukio hilo ambalo limefanywa na klabu ya Madrid, klabu yetu na mashabiki kwa sasa wanasubiri ripoti hiyo ili kuona hatua gani zitachukuliwa.
“Nilipitia wachezaji wote ambao wamesimamishwa baadhi ya michezo msimu huu, lakini tulishangaa kuona Madrid wakimtumia mchezaji huyo ambaye hakutakiwa kutumika,” alisema Vizcaino.

 

Hata hivyo, baada ya Madrid kugundua kwamba wamefanya kosa kumchezesha mchezaji huyo waliamua kumtoa katika kipindi cha pili cha mchezo huo na nafasi yake ikichukuliwa na Mateo Kovacic.

Septemba mwaka huu, klabu ya Osasuna ilitolewa katika michuano hiyo kwa kosa kama hilo la kumtumia Unai Garcia, ambaye alitakiwa kutumikia kadi ambayo alioneshwa msimu uliopita kwenye mchezo dhidi ya Mirandes.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles