26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

REA: Zaidi ya Vijiji 1300 Tanzania bara vimepata umeme

Derick Milton, Simiyu

Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imesema jumla ya vijiji 1,310 kati ya 3,559 Tanzania Bara, tayari vimepata umeme kupitia mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu mzungumko wa kwanza ambao unagharimu takribani kiasi cha sh trilioni 1.2.

Mradi huo ambao ulianza utekelezaji wake Julai, 2018 unatarajiwa kukamilika Juni 2020, ambapo REA imesema kuwa wanatarajia kupata takribani wateja laki mbili.

Hayo yameelezwa na Kaimu na Mkurugenzi wa uendelezaji wa masoko na Teknolojia REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati akiongea na Mtanzania Digital kwenye maonesho ya sikuu ya wakulima yanaonedelea kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Amesema vijiji hivyo ambavyo vimefikiwa na mradi tayari wamewashiwa umeme na wakandarasi wote wanaendelea na kazi ya kuhakikisha mradi huo unakamilika mwaka 2020.

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuvifikia vijiji vyote 12,268 tanzania bara ifikapo mwaka 2021, na kuviwekea umeme huku katika Mkoa wa Simiyu mradi huo ukifikia asilimia 66 ya utekelezaji wake.

Amesema kuwa katika mkoa wa Simiyu wanatarajia kufikia takribani vijiji 152 kupitia mradi huo na wateja 7000 kwa gharama ya sh. bilioni 34.2.

“Mradi huu mbali na kuwafikia wananchi wengi sasa hivi, umefanikisha kuanzishwa kwa viwanda vya nguzo za umeme kutoka vitatu hadi tisa, Mita za umeme kutoka 0 hadi 4, Transfoma 1 hadi 4, na Waya kutoka 1 hadi 5,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles