24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

RC Shigela asimamisha watumishi 8 TRA

NA OSCAR ASSENGA,MKINGA

MKUU wa  Mkoa wa Tanga, Martin Shigela amewasimamisha kazi watumishi 8 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kituo cha Horohoro wilayani Mkinga, huku akiamuru Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Daudi Mwafwimbo kuwakamata na kuweka chini ya ulinzi.

Uamuzi huo,umekuja baada ya kuundwa  kamati ya uchunguzi kituoni hapo kwa madai ya watumishi hao kufanya kazi zao wakiwa na tuhuma mbalimbali ndani na nje ya kituo.

Kabla ya kutoa uamuzi huo jana, Shigela aliishukuru kamati  na kueleza kuwa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili watumishi hao, kuwa  ni pamoja na malalamiko ya wafanyabiashara kuzuiwa mizigo na kuomba rushwa, kupitisha mifugo kwa njia za panya na mengineyo.

“Kwanza niishukuru  kamati, kituo cha Horohoro ndiyo kituo mama kwa upande wetu, kuna baadhi ya watumishi wamekigeuza shamba la bibi kila mmoja anafanya anavyotaka.

“Nawambia wananchi, Serikali ya awamu ya tano haitaki kuona mwananchi anaonewa na mtumishi wala mtumishi anaonewa na mwananchi, tume imefanya kazi yake vizuri na imetoa majibu mazuri,”alisema.

Aliwataja watumishi waliosimamishwa, kuwa ni Edward Meneja wa Forodha Mkoa wa Tanga, Ofisa Forodha Mfawidhi wa kituo hicho, Bakari Athumani, Ofisa Forodha Msaidizi, Danda Hamis na Ofisa Forodha Msaidizi, Azizi Dutiro.

Wengine ni Ofisa Forodha Julius Asila, Bakari Ngoso Ofisa Forodha Msaidizi wa kituo, Nicodem Kilahuzi, Ofisa Mifugo na Michael Katamba Ofisa Mkaguzi wa  Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Katibu wa kamati ya uchunguzi, Horombo Alexander alisema uchunguzi umefanyika ndani ya miezi mitatu,ulianza Septemba 18 na kumalizika mwezi huu.

Alisema uchunguzi umebaini upungufu mwingi ambayo mengine yameanza tangu kuanzishwa kwa kituo hicho hasa kuhusu suala la kupitisha mifugo kwa njia za panya kuingia nchi jirani ya Kenya.

“Ukiwauliza mifugo inapitishwa wapi hapa forodhani wanakwambia hawajui na kituo hiki hakijawahi kuingiza mapato ya mifugo licha ya kuwa mifugo inapitishwa kila siku kutoka Tanzania kwenda kuuzwa nchi jirani ya Kenya, huku mpakani hakuna wanachojua”

Alisema katika kituo hicho kumefungwa mashine za scanner ambayo baada ya kuifanyia uchunguzi waligundua hainasi dawa za kulevya wala fedha bandia, huku zikiwa zikisimamiwa na watumishi wa TRA pekee.

“Baada ya kugundua mapungufu katika scanner hii, tumeona tuongeze watumishi wa idara nyingine kuja kusimamia nao, tumeleta hapa idara ya polisi,usalama, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji, afya na TRA yenyewe,” alisema.

“Tumegundua madudu mengi katika kituo kwa upande wa mifugo,ofisa wa kituo cha mifugo hana taarifa ya kueleweka isipokuwa ana kitabu chake chenye taarifa zake hashirikishi mtu” aliongeza.

Aliiomba Serikali kuwachukulia hatua kali watumishi wote waliohusika katika ubadhirifu wa mali za taifa kwa maslahi yao binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles