Neema Paul, TUDARCO
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel amemuahidi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutekeleza maagizo ya serikali ikiwemo kuzingatia na kujali ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa kuitumikia serikali na kupiga vita rushwa.
Gabriel ameyazumgumza hayo leo Septemba 8, wakati akifanya utambulisho wa viongozi mbalimbali waliohudhuria tamasha la utamaduni lililofikia kilele chake hii leo jijini Mwanza.
Ameahidi kuwa na utumishi uliotukuka kwa Wananchi, kupiga vita rushwa na kuongeza mapato ya serikali ili kutekeleza miradi mbalimbali yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla.
Aidha katika maadhimisho hayo Rais Samia amewapongeza umoja wa machifu wa kisukuma wa mkoa wa Mwanza kwa kuandaa tamasha hilo huku akitoa wito kwa makabila yote ya Tanzania kuanza kutangaza mila na desturi zao.