26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 3, 2024

Contact us: [email protected]

RC Mwanza aahidi utumishi uliotukuka

Neema Paul, TUDARCO

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel amemuahidi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  kutekeleza maagizo ya serikali ikiwemo kuzingatia na kujali ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa kuitumikia serikali  na kupiga vita rushwa.

Gabriel ameyazumgumza hayo leo Septemba 8, wakati akifanya utambulisho wa viongozi mbalimbali waliohudhuria tamasha la utamaduni lililofikia kilele chake hii leo jijini Mwanza.

Ameahidi  kuwa na utumishi uliotukuka kwa Wananchi, kupiga vita rushwa na kuongeza mapato ya serikali ili kutekeleza miradi mbalimbali yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla.

Aidha katika maadhimisho hayo Rais Samia amewapongeza umoja wa machifu wa kisukuma wa mkoa wa Mwanza kwa kuandaa tamasha hilo huku akitoa  wito kwa makabila yote  ya Tanzania kuanza kutangaza mila na desturi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles