24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

RC MTAKA AMWOMBA WAZIRI KUWATUMBUA WATUMISHI WATATU

Na DERICK MILTON-SIMIYU

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka, amemwomba Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, kuwatumbua  watumishi watatu wa Halmashauri ya Bariadi mkoani humo kwa kosa la uzembe wa kupindukia.

Watumishi hao ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Abdallah Malela, Ofisa Ardhi wa halmashauri hiyo, Mazengo Sabaya pamoja na Ofisa Ardhi wa Mkoa wa Simiyu, Grace Ngombela.

Watumishi hao wanadaiwa kushindwa kutoa hati miliki za kimila za mashamba  zaidi ya 60,000 ya wananchi  tangu mwaka 2008 kupitia mradi wa hati na vyeti vya ardhi ya kijiji ulipoanzishwa katika halmashauri hiyo.

Hata hivyo, ombi la Mtaka lilikataliwa na Mabula na kusema kwamba anayepaswa kuchukuliwa hatua ni Ofisa Ardhi wa Mkoa wa Simiyu, Grace Ngombela, ambaye ameshindwa kuwasimamia watu wake na kusababisha hali hiyo ya uzembe ambao umesababisha malalamiko ya wananchi.

Awali, Mabula alisema wananchi wengi wamelalamika kutopewa hati zao kwa muda mrefu huku Halmashauri ya Bariadi  ikiwa imekaa na hati  bila ya kuwapatia wamiliki wake.

Pia Mabula alisema ameshangazwa na kitendo cha watumishi hao kushindwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika juu ya sababu za kushindwa kutolewa kwa hati hizo.

“ Nimekuja hapa nataka maelezo ya kutosha kutoka kwa mkurugenzi na maofisa ardhi wake, kwanini wamekaa na lundo la hati katika ofisi zao na hazijatolewa kwa wananchi, kwanini hawajatoa sababu  katika mamlaka husika badala yake mmenyamaza,” alihoji Mabula.

Akijibu maswali hayo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Abdallah Malela, alikiri kuwepo kwa hati hizo na kusema kuwa sababu kubwa ni kutokana na halmashauri hiyo kugawanywa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles