24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

MWANJELWA ATAKA UCHUNGUZI UFANYWE KUBAINI WEZI SACOSS

Na Mathias Canal- Mbeya

NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa, amemwagiza Mrajisi Mkuu wa Maendeleo ya Ushirika nchini, kuanza uchunguzi mara moja kwenye Saccos ya wakulima wa mpunga Madibira iliyoko wilayani Mbarali, mkoani Mbeya.

Hatua hiyo inalenga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watendaji waliohusika na upotevu wa fedha pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Dk. Mwanjelwa alitoa agizo hilo juzi wakati akipokea taarifa ya kilimo ya Wilaya ya Mbarali akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune, alimweleza Mwanjelwa kuwa katika Saccos ya Madibira kumekuwa na hasara kubwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika.

Hivyo alimwomba Naibu Waziri kuwachukulia hatua za kinidhamu haraka viongozi wote waliosababisha hasara kwenye vyama hivyo vya ushirika baada ya uchunguzi kufanyika katika kipindi cha siku 14.

Aliongeza kuwa taarifa ya ukaguzi iliwasilishwa kwa Mrajisi wa vyama vya ushirika kwa barua Kumb Na. MDC/C.20/10/89 tarehe 23/01/2017, lakini mpaka sasa hazijachukuliwa hatua zozote za kinidhamu jambo ambalo linafifisha shughuli za wananchi kujipatia maendeleo endelevu.

Dk. Mwanjelwa ametoa wiki mbili kwa Mrajisi kufika katika Saccos hiyo ya Madibira na kutoa majibu haraka ya matokeo ya uchunguzi huo katika kipindi tajwa.

Alisema viongozi wa wilaya zote nchini wana jukumu muhimu la kuhamasisha na kuhimiza wanachama kuongeza thamani ya mitaji yao ili kuviwezesha vyama kukuza mitaji ya ndani badala ya kuwa tegemezi kwenye taasisi nyingine za kifedha.

Aidha, kuendelea kutoa elimu juu ya mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani ili mkulima apate bei stahiki ya mazao yake.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles