30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

RC MGHWIRA AONYA WINGI WA MIFUGO

 

Na SAFINA SARWATT

  • MOSHI

WAFUGAJI jamii ya Wamaasai mkoani Kilimanjaro, wameshauriwa kupunguza  idadi ya  mifugo waliyonayo ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira na migogoro ya ardhi  baina yao na wakulima.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira,

wakati akizungumza na  wananchi wa jamii ya Wamaasai wa Kata ya Mabogini

wilayani Moshi Vijijini, katika zoezi la  kubadilishana rika kutoka

vijana kwenda uzee.

Alisema kuna haja ya jamii hiyo kuanza kufuga kisasa na kupunguza

idadi ya makundi makubwa ya mifugo ambayo yamekuwa yakiharibu mashamba ya wakulima na kusababisha migogoro ya mara kwa mara.

 

“Kuna haja ya  viongozi wa vijiji hivyo kuandaa mpango mkakati wa

kusaidia jamii hiyo ya wafugaji kuwa na shughuli mbadala za kuwaingiza kipato  pamoja na idadi ndogo ya mifugo kwa kuwa ongezeko la watu limesababisha uhaba wa ardhi,” aliongeza.

kwa upande wake Diwani wa kata hiyo,  Emmanuel Mzava, alisema

wameanza utaratibu wa kutenga maeneo ambayo hayajaendelezwa kwa

ajili ya malisho pamoja  na kuunda kamati  za  kudhibiti makundi ya mifugo yanayokaa mbali na kuingizwa kwenye mashamba ya wakulima.

 

Baadhi ya wafugaji walieleza  adha kubwa wanayoipata kipindi cha

kiangazi kuhama na makundi ya mifugo kwa ajili ya kutafuta malisho

katika mikoa jirani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles