27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

HAKIMU ANG’AKA DPP KUTUMIA SHERIA ‘KWA RAHA ZAKE’

Na JANETH MUSHI

-ARUSHA

HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Nestory Baro amesema nguvu ya kisheria aliyonayo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), haipaswi kutumiwa kwa raha zake.

Hakimu Baro ametoa onyo hilo mahakamani leo Agosti 30, mjini hapa kabla ya kuifuta kesi ya inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya anayetuhumiwa kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa ambayo ilikuja mahakamani hapo leo kwa ajili ya kutajwa.

“Huu umekuwa ni mchezo wa Jamhuri kufuta kesi hiyo namba 284 ya mwaka huu kila mara na kuirudisha mahakamani tena jambo ambalo ni matumizi mabaya ya mamlaka iliyopewa ofisi hiyo.

“Sheria inakataza nguvu alizopewa DPP asitumie kwa raha zake, akiamka tu usingizini anasema kuanzia leo Sabaya sijui nini. Huu mchezo wa kumkamata mtu kumleta mahakamani na kumrudisha, mtaufanya hata mara milioni, sheria inaruhusu huu mchezo?  nataka iwe mwisho hii nenda rudi,” amesema.

Hata hivyo, Hakimu Baro alimuuliza Wakili wa Serikali, Penina Joachim sababu za kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo ambapo Wakili huyo alidai sheria haimlazimishi kueleza sababu za kutokuendelea na kesi mahakamani.

“Penina nataka ukomae kidogo, sheria hairuhusu huu ujinga, ukitumwa siku nyingine kuja kusema hamna nia ya kuendelea na kesi uulize na sababu siyo uje hapa mahakamani useme upande wa upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na kesi, why? (kwanini)” alihoji Hakimu Baro.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles