27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

RC Kilimanjaro: nzige walioonekana Moshi wametoweka

Upendo Mosha, Moshi

Mkuu wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amethibitisha uwepo wa nzige walioonekana jana jioni katika Wilaya ya Moshi na baadaye kutoweka.
Amesema wataalamu wakiwamo wa afya ya mimea wapo kazini kufuatilia hali hiyo ili kujiridhisha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 10, Mghwira baada ya uvumi wa uwepo wa nzige wataalamu wa afya ya mimea walifika katika maeneo ya Moshi na kwamba taarifa zaidi zitatolewa.

“Nzige hao kwa sasa hawapo na wataalamu wapo maeneo mbalimbali ya Mkoa Kilimanjaro na kujiridhisha.

“Kulitokea uvumi wa uwepo wa nzige katika maeneo ya Mwanga na mpakani walikuwa kilometa 50, lakini baadaye walionekana Wilaya ya Moshi na kisha wakatoweka kwa hiyo ni Kama walikuwa wanapita,” amesema.

Aidha amesema kwa sasa Kuna vipepeo vingi sana katika maeneo mbalimbali ya Moshi ambapo aliwasiliana na wataalamu kutoka Kenya na walimueleza wamechukua sampuli kuwapima kama wana uhusiano na nzige.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles